Sura 34 · dakika 5 za kusoma
Kuvuna Roho
Matunda ya mwenye haki ni mti wa uzima, naye avutaye roho za watu ni mwenye hekima.” Mithali 11: 30.
Katika makala katika The Student Movement ya Februari 1901, juu ya “Kuamka kwa Kiroho,” iliyoandikwa na H. W. Old-ham, nimekuta sentensi zifuatazo: “Katika katiba za Vyama vingi vya Kikristo vya Wanafunzi imeelezwa ya kuwa lengo kuu la Chama cha S.C. ni kuwaongoza wanafunzi kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo. Lakini kama swali litasukumwa hadi mwisho, ‘Je, wanafunzi kweli wanavutwa kutoka katika kutojali na kutokuamini hata kuwa na imani katika Yesu Kristo?’ jibu ni lazima liwe ya kuwa, ijapokuwa katika visa vichache ndivyo ilivyo, katika Vyama vingi ni jambo la mashaka makubwa. Vyama vingine, vikivunjika moyo kwa kushindwa kuliopita, vimekuwa na shaka juu ya uwezekano wa kuwavuta watu kwa Kristo katika mazingira magumu kama yao wenyewe. Vyaweza kuendeleza kwa kiasi fulani mbinu za kienyeji za kazi ya kushambulia, lakini vimeacha kutarajia kufanya zaidi ya kuwatia nguvu wale walio na imani tayari.
Halmashauri Kuu ya Idara ya Vyuo imeweka kwa hakika kuamka kwa kiroho kwa wanafunzi mstari wa mbele wa sera yao. Kama Vyama vya mtaa vitajikusanya kuizunguka Halmashauri twaweza kutarajia kikamilifu kumwona Mungu akitenda kazi katika maisha ya wale wanaotuzunguka.
‘Upendo uliotuvuta sisi waweza kuwavuta wengi. Ni sawa kutambua uzito wa kuchukua lengo hili. Lahusisha ushirika wa karibu na Yesu Kristo katika maisha matakatifu, katika kujitoa sadaka, katika huduma ya upendo; lataka kunyenyekea marekebisho na uongozi wa Roho wa Mungu…Ni lazima tuliinue lengo la kuwavuta wanafunzi kwa Kristo kutoka nyuma katika kazi yetu na kuliweka la kwanza. Vyama vyetu vina watenda kazi wa kimitambo wa kutosha na kupita kiasi. Vyahitaji wanaume na wanawake wenye malengo dhahiri, watakaofikiri na kuomba, na kuomba na kufanya kazi mpaka Chama chao kiwe chombo kifaacho katika mkono wa Mungu cha kubadilisha maisha ya wanafunzi.”
Katika Tahariri katika toleo lilo hilo, twasoma kuhusu Siku ya Maombi, “Kuna maungamo mengi, na maombi mengi ambayo itatupasa kuyafanya katika siku ya maombi; lakini kwa nafsi zetu, twahisi ya kuwa la dharura kuliko yote ni lazima liwe ombi la kuamka kwa kiroho. Tumekuwa tukilitambua taratibu jambo la kuwa Vyama vyetu vingi havivuti watu kwa Kristo, na vingine vimeanza kutambua kwa fadhaa ya kuwa jambo hilo limevisababishia huzuni ndogo sana. ‘Ni bahati mbaya kwa hakika ya kuwa wanafunzi hawajavutwa, lakini — twaweza kufanya nini? Kwa kweli kuamka kwa kiroho kwahitajika; kwahitajika katika mioyo yetu wenyewe. Kutakapokuja tutagundua upesi la kufanya. Iko wapi ile shauku yenye moto ya kuwasaidia watu? Liko wapi lile ombi la dharura kwa ajili ya ndugu yetu ambalo halitakataliwa?
Katika kiini chenyewe cha jambo lote ni kukosa kwetu kupendezwa. Ni kile tu kinachotupendeza kitakachowavuta watu.
Ni pale tu chini kabisa miongoni mwa mahangaiko ya milele ya nafsi yetu unapowaka tamaa yenye shauku ya kuwaongoza watu kwa Kristo, ndipo tutakapokutana na wale wahitajio msaada wetu, na watakaoukaribisha. Ni maneno na matendo yale tu yalipukayo kutoka katika shauku iwakayo ya tamaa ya kuwasaidia watu, ndiyo yapatayo nafasi za kuathiri maisha. Kwa maana ni pale tu palipo na tamaa kama hii, ndipo tunapotambua ya kuwa pasipo yeye hatuna nguvu, ama kuwapata wale wahitajio au, tukiisha wapata, kuwapa msaada. Je, hatutaomba pamoja ya kuwa shauku kwa ajili ya roho ipate kuzaliwa ndani ya kila mmoja wetu katika siku ya maombi?”
Kwa hili na niongeze nukuu kutoka katika makala juu ya “Mahitaji ya India,” katika toleo la Januari la gazeti lilo hilo. Mwandishi (Mch. W. E. S. Holland, hapo awali Katibu wa Safari wa B.C.C.U.) alikuwa amenena juu ya kusudi kuu katika kuanzishwa kwa Vyuo vya Umisheni kuwa ni “ushawishi binafsi ambao waalimu katika vinne vya Vyuo vikubwa zaidi vya Umisheni vya India ambao wakati wao unatumika kikamilifu hivyo kwa kufundisha hata hawana wakati wala roho ya umoja binafsi na wanafunzi wao. Saa tano au sita kwa siku, pamoja na kadhaa zaidi katika maandalizi, katika hali ya hewa ya India, humwacha mtu amechoka, bila wakati wala nguvu ya neva kwa ajili ya ile kazi iliyo nzito kuliko zote, kushughulika na mtu mmoja mmoja kuhusu nafsi yake.”
Ahitimisha makala yake kwa maneno haya: “Watu 40,000 wahitajika, si pungufu kama India yote itasikia. Na hata hivyo mtu karibu ajikute anasita kutoa ombi la watu. Kwa nini? Ili watu wasije wakawa mzigo kwa ardhi. Kwa maana kazi ya umisheni ni, hatimaye, ni kuvuna roho tu. Na hakuna kitu kimfanyacho mtu kuwa mvunaji wa roho India ambaye hajakuwa mvunaji wa roho nyumbani.
Fahamu ya wajibu, au ya hitaji kuu, yaweza kumleta mtu India. Hakuna kiwezacho kumwezesha kuishi mwaka baada ya mwaka maisha ya umisheni huku, ila upendo wenye moto kama huo kwa Kristo ulazimishao kujitoa sadaka na maisha ya kuvuna roho nyumbani.”
Ni mawazo gani nukuu hizi huyapendekeza kuhusu kazi ya kuvuna roho! Ya kuwa ndilo hitaji kuu la kwanza katika mmisheni. Ya kuwa kwenda kwenye uwanja wa umisheni hakutamfanya kwa hakika mtu kuwa mvunaji wa roho. Ya kuwa ni nyumbani, kabla mtu haingii katika uwanja wa umisheni, ndipo roho ya kujitoa sadaka na kuvuna roho ni lazima ipatikane na kuzoezwa. Kuwazoeza wanachama wake katika ustadi wa kuvuna roho ni mojawapo ya malengo makuu ya Vuguvugu la Wanafunzi, kama vile kulitenda kutakuwa kipimo cha nguvu yake na mafanikio yake. Ya kuwa hatari hutisha daima ya sisi kuporomoka kutoka katika hili kuingia katika mbinu za kienyeji na za kimitambo. Ya kuwa maombi ya daima, yenye moto, ya pamoja, na ya faragha yapaswa kufanywa kwa ajili ya upendo zaidi kwa roho, na jitihada za daima, za bidii, za pamoja, na za faragha zitolewe katika kila Chama cha Wanafunzi ili wenzetu wapate kuvutwa kwa Kristo.
Sifa kuu ya uzima wa Kimungu, ikiwa ndani ya Mungu, ndani ya Kristo, au ndani yetu, ni — upendo utafutao kuwaokoa waliopotea. Haya na yawe maisha ya Kikristo tuyakuzayo; upendo upatao heri yake katika kuwaokoa wanadamu. Uzima huu haukuzwi kwa mtu kwa namna nyingine yoyote ila kwa kushikamana kwa karibu binafsi na Yesu, na ushirika wa kila siku naye kama Rafiki tumpendaye.
Ni katika chumba cha ndani ndipo ushirika huu na Baba na Mwana upaswapo kudumishwa. Ni katika hili ndipo Baba atuonaye sirini atatujazi kwa dhahiri.