Sura 27 · dakika 4 za kusoma
Kufanywa Upya Kwa Kila Siku — Mfano
Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.” — Wakolosai 3: 9-10.
“Ikiwa mmemsikia yeye, na kufundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.” Waefeso 4: 21, 23, 24.
Katika kila jitihada, ni jambo la maana kuwa na lengo lililowekwa waziwazi. Haitoshi ya kuwa kuna mwendo na maendeleo, twataka kujua kama mwendo ni katika mwelekeo ulio sahihi, moja kwa moja kwenye lengo; na hasa tunapotenda katika ushirika na mwingine, ambaye twamtegemea, twahitaji kujua ya kuwa lengo letu na lake ziko katika upatano kamili. Kama kufanywa upya kwetu kwa kila siku kutafikia lengo lake twahitaji kujua waziwazi na kushika imara kile kusudi lake kilicho.
"Mmevaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu." Uzima wa Kimungu, kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu, si nguvu ya upofu, kama katika asili. Twapaswa kuwa watenda kazi pamoja na Mungu; ushirikiano wetu wapaswa kuwa wa akili na wa hiari, "Utu mpya unafanywa upya siku kwa siku upate ufahamu." Kuna ufahamu ambao akili ya asili yaweza kuutoa katika Neno, lakini usio na uzima na nguvu, ile kweli halisi na kiini, viletwavyo na ufahamu wa kiroho.
Ni kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu kutoako ufahamu wa kweli, ambao haukai katika wazo na dhana, bali katika kuonja kwa ndani, mapokezi yaliyo hai ya vitu vyenyewe ambavyo maneno na mawazo ni taswira zavyo tu. “Mmevaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu” Hata kujifunza kwetu Biblia kukiwa kwa bidii kiasi gani, hakuna ufahamu wa kweli upatikanao zaidi ya kadiri ambayo kufanywa upya kwa kiroho kunavyoonjwa; "kufanywa upya katika roho ya nia," katika uzima wake na nafsi yake ya ndani, peke yake ndiko kuletako ufahamu wa kweli wa Kimungu.
Na sasa ni mfano gani utakaofunuliwa kwa ufahamu huu wa kiroho utokao katika kufanywa upya kama lengo lake la kweli na pekee? Utu mpya unafanywa upya upate ufahamu, sawasawa na Mfano wake Yeye Aliyeuumba. Si kitu pungufu ya sura, mfano wa Mungu. Hilo ndilo lengo moja la Roho Mtakatifu katika kufanya kwake upya kwa kila siku; hilo lapaswa kuwa lengo la mwamini atafutaye kufanywa upya huko.
Hili ndilo lilikuwa kusudi la Mungu katika uumbaji, "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu." Ni kwa kiasi kidogo kiasi gani utukufu usio na kikomo wa maneno haya hufikiriwa. Ni kwa kisicho pungufu ya hili, Mungu alipuliza uzima wake mwenyewe ndani ya mwanadamu, ili upate kuzalisha ndani ya mwanadamu duniani mfano mkamilifu wa Mungu mbinguni? Katika Kristo, sura hiyo ya Mungu imefunuliwa na kuonekana katika umbo la kibinadamu. "Tumekwisha kukusudiwa tangu asili na kukombolewa na kuitwa, twafundishwa na kufanywa na Roho Mtakatifu, ili tufananishwe na sura ya Mwana, kuwa wafuasi wa Mungu, na kuenenda kama vile Kristo alivyoenenda. Kufanywa upya kwa kila siku kwaweza kuendeshwaje, kujifunza kwa kila siku Biblia na maombi kwaweza kufaa nini, tusipoweka moyo wetu juu ya kile Mungu ameuweka wake,” Utu Mpya Ukifanywa Upya Siku Kwa Siku Sawasawa na Mfano wake Yeye Aliyeuumba.
Katika kifungu cha pili, tunalo wazo lilo hilo lililoelezwa kwa namna tofauti kidogo. Mfanywe wapya katika roho ya nia yenu, na mvae utu mpya, ambao sawasawa na Mungu kwa kadiri ya mfano wa Mungu, umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli. Haki ni chuki ya Mungu juu ya dhambi, na kudumisha kwake yaliyo sahihi. Utakatifu ni utukufu wa Mungu usioelezeka, katika upatano mkamilifu wa haki yake na upendo wake. Kuinuliwa kwake kusiko na mwisho juu ya kiumbe. Muungano wake mkamilifu naye. Haki katika mwanadamu inajumuisha mapenzi yote ya Mungu kuhusu wajibu wetu kwake au kwa wenzetu: utakatifu ni uhusiano wetu binafsi naye mwenyewe. Kama vile utu mpya ulivyoumbwa, ndivyo unavyopaswa kufanywa upya kila siku, sawasawa na Mungu katika haki na utakatifu wa kweli." Ni ili kuhakikisha hili ndipo nguvu ya Roho Mtakatifu itendayo kazi ndani yetu. Ni ili kuhakikisha hili ndipo atungojea siku kwa siku ili tujitoe kwake, katika neema yake na nguvu yake ya kufanya upya.
Saa ya asubuhi irudiyo kila siku ndio wakati wa kuhakikisha kufanywa upya kwa kila siku kwa Roho Mtakatifu kuwa sura ya Mungu kama haki na utakatifu wa kweli. Ni jinsi gani lahitajika kutafakari na kuomba ili kuuweka moyo juu ya kile Mungu akilengalo, na kupata maono ya kweli ya uwezekano ule wa ajabu: utu wa ndani ukifanywa upya siku kwa siku hata kuwa mfano hasa wa Mungu, ukigeuzwa kuwa sura iyo hiyo, kama kwa Roho wa Bwana. Mwanafunzi Mkristo!
Kisicho pungufu na kiwe lengo lako, wala kikidhi shauku zako. Sura ya Mungu, uzima wa Mungu umo ndani yako. Mfano wake waweza kuonekana ndani yako. Usimtenganishe tena Mungu na mfano wake, kila mmoja na amwendee, wote na wamtegemee, kusimaanishe kisicho pungufu ya kumpata yeye, katika mfano wake uliofanyizwa ndani yako kwa kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu. Hili na liwe ombi lako la kila siku, kufanywa upya sawasawa na sura yake yeye aliyekuumba.