Sura 22 · dakika 5 za kusoma
Mapenzi ya Mungu
Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni." — Mathayo 6: 10.
1. Mapenzi ya Mungu ndiyo nguvu iliyo hai ambayo kwayo ulimwengu wadaiwa kuwako kwake. Kwa mapenzi hayo, na kwa kadiri ya mapenzi hayo, ulimwengu ni ulivyo. Ni usemi au dhihirisho au mfano wa mapenzi ya Kimungu katika hekima yake, nguvu yake na wema wake. Wenye, katika uzuri na utukufu, ni kile tu unachodaiwa kwa Mungu kuwa aliutaka. Kama vile mapenzi hayo yalivyouumba, ndivyo yauhifadhivyo kila siku. Hivyo uumbaji hufanya ule uliokusudiwa kwa ajili yake, waonyesha utukufu wa Mungu. “Wale wenye uhai humpa yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai milele na milele, kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”
2. Hili ni kweli kwa asili isiyo na uhai. Ni kweli zaidi hata kwa viumbe wenye akili. Mapenzi ya Kimungu yalichukua kazi ya kuumba kiumbe katika sura na mfano wake yenyewe, chenye nguvu iliyo hai ya kujua na kukubali na kushirikiana na Mapenzi yale ambayo kwayo kiumbe kilidaiwa kuwako kwake. Heri ya malaika wasioanguka yakaa katika kuhesabu kuwa heshima na furaha yao ya juu kabisa kuweza kutaka na kutenda sawasawa yale ambayo Mungu ayataka na ayatenda. Utukufu wa mbinguni ni kwamba mapenzi ya Mungu hutimizwa huko.
Dhambi na taabu ya malaika na wanadamu walioanguka yakaa tu katika wao kuwa wamejigeuza na kukataa kukaa katika, na kutenda, mapenzi ya Mungu.
3. Ukombozi si kitu kingine ila kurudishwa kwa mapenzi ya Mungu mahali pake katika ulimwengu. Kwa mwisho huu, Kristo alikuja na kuonyesha katika maisha ya kibinadamu, jinsi mwanadamu alivyo na jambo moja tu la kuishi kwa ajili yake, kutenda mapenzi ya Mungu. Alituonyesha jinsi ilivyokuwa na njia moja ya kushinda utashi binafsi — kwa kuufia, katika kutii mapenzi ya Mungu hata mautini. Hivyo aliufanyia upatanisho utashi wetu binafsi na kutushindia sisi, na kufungua njia kupitia mauti na ufufuo, kuingia katika uzima ulioungana kabisa na, na kujitoa kwa, mapenzi ya Mungu.
4. Mapenzi ya Mungu ya ukombozi sasa yaweza kutenda ndani ya mwanadamu aliyeanguka, yale ambayo mapenzi yake ya uumbaji yalitenda na daima hutenda katika asili, au ndani ya viumbe wasioanguka. Katika Kristo na kielelezo chake, Mungu amefunua kujitoa kwa na furaha katika mapenzi yake, ayaombayo na ayatarajiayo kwetu. Katika Kristo na Roho wake huufanya upya na kuumiliki utashi wetu: hutenda kazi ndani yake kutaka na kutenda, akitufanya kuwa na uwezo na utayari wa kuyatenda mapenzi yake yote. Yeye mwenyewe hufanya mambo yote kwa kadiri ya shauri la mapenzi yake. “Awakamilishe katika kila neno jema, mpate kuyatenda mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu yapendezayo mbele zake.” Kadiri hili linavyofunuliwa na Roho Mtakatifu, kuaminiwa, na kupokewa ndani ya moyo, twaanza kupata ufahamu wa ndani wa lile ombi, “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.” nayo tamaa ya kweli huamshwa kwa ajili ya uzima uahidio.
5. Ni jambo la lazima kiasi gani kwa mwamini kutambua uhusiano wake na mapenzi ya Mungu na dai layo juu yake. Waaminio wengi, wengi sana, hawana wazo lolote la yale ambayo imani yao au hisia yao yapaswa kuwa kuhusu mapenzi ya Mungu. Ni wachache kiasi gani wasemao: Wazo langu lote la heri lakaa katika kitu kisicho kingine ila upatano ulio kamili kabisa na mapenzi ya Mungu. Nahisi hitaji langu moja kuwa, kujisalimisha kunakodumishwa daima, ili, hata katika jambo dogo kabisa, nisitende kamwe zaidi ya yale Mungu anitakayo niyatende. Kwa neema ya Mungu, kila saa ya maisha yangu yaweza kuwa kuishi ndani ya mapenzi ya Mungu, na kuyatenda kama yatimizwavyo mbinguni.
6. Ni pale tu imani iliyo hai katika Mapenzi ya Kimungu, ikitimiza makusudi yake kwa kuzidi ndani yetu, iumilikipo moyo, ndipo tutakuwa na ujasiri wa kuamini jibu la lile ombi Bwana wetu alilotufundisha. Ni pale tu tuonapo, ya kuwa ni kwa njia ya Yesu Kristo kufanya kazi huku kwa mapenzi ya Mungu ndani yetu kwatimizwa, ndipo tutakapoelewa jinsi ni ule muungano wa karibu naye utoao hakika ya kuwa Mungu atatenda vyote ndani yetu. Nayo ni hakika hii tu katika Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, itakayotuhakikishia, ya kuwa sisi nasi twaweza kutenda fungu letu, na ya kuwa utashi wetu dhaifu duniani waweza kweli daima kupatana na kushirikiana na mapenzi ya Mungu. Na tukubali kusudi letu na wajibu wetu kama jambo lile moja moyo wetu utamanilo, ya kuwa katika kila kitu mapenzi ya Mungu yatimizwe ndani yetu na kwa sisi, kama yatimizwavyo mbinguni; imani hiyo itaushinda ulimwengu.
7. Utashi hauwezi kutenganishwa na muungano wake ulio hai na Baba hapa, wala na uwepo ulio hai wa Mwana Aliyebarikiwa. Ni kwa uongozi wa Kimungu utolewao kwa njia ya Roho Mtakatifu peke yake, ndipo mapenzi ya Mungu katika uzuri wake, katika utumizi wake kwenye maisha ya kila siku, katika ufunuo wake ukuao daima, yaweza kujulikana kweli. Fundisho hili litatolewa, si kwa wenye hekima na akili, bali kwa watoto wachanga, watu wenye tabia ya kitoto, walio tayari kungoja na kutegemea yale wapewayo. Uongozi wa Kimungu utaongoza katika njia ya mapenzi ya Mungu.
8. Umoja wetu wa siri na Mungu ndio mahali tunapoyarudia na kuyajifunza yale mafunzo makuu… Mungu nimwabuduye huniomba muungano mkamilifu na mapenzi yake… Ibada yangu yamaanisha: “Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu” Saa ya asubuhi, chumba cha ndani, umoja wa siri na Mungu, kama katika haya ujuzi wa mapenzi ya Mungu, nguvu ya kuyatenda, kujisalimisha kote na kwa furaha kufanya yote Mungu ayatakayo, unavyotafutwa na kukuzwa, kujifunza kwetu neno la Mungu na maombi yetu kutaleta baraka yake ya kweli na kamili.