Sura 3 · dakika 3 za kusoma

Tofauti Ya Roho Mtakatifu Na Baba Na Mwanawe, Yesu Kristo

Sura hii yaeleza kwamba Roho Mtakatifu si sawa na Baba wala Mwana — Yeye ni Nafsi tofauti. Biblia laonyesha hili waziwazi katika masimulizi kama ubatizo wa Yesu na ahadi yake ya kumtuma Roho Mtakatifu. Wote watatu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni tofauti, lakini ni Mungu kamili, nao hutenda kazi pamoja katika umoja.

Tumeona hadi sasa kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi tena Nafsi ya Kimungu. Na sasa swali lingine lazuka, je, kama Nafsi yu tofauti na wa peke yake mbali na Baba na Mwana? Yeye achunguzaye kwa makini maneno ya Agano Jipya hana budi kugundua kwamba bila shaka yu hivyo. Twasoma katika Luka 3:21-22, 'Ikawa, watu wote walipokuwa wakibatizwa, na Yesu naye amebatizwa, akawa anaomba, mbingu zikafunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, nimependezwa nawe.'

Hapa tofauti iliyo wazi kabisa yachorwa kati ya Yesu Kristo, aliyekuwa duniani, na Baba aliyenena naye kutoka mbinguni kama nafsi anenavyo na nafsi nyingine, na Roho Mtakatifu aliyeshuka kwa mfano wa kiwiliwili kama hua kutoka kwa Baba, aliyekuwa akinena, kwa Mwana, aliyekuwa akiambiwa, na kutulia juu ya Mwana kama Nafsi tofauti na wa peke yake mbali naye. Twaona tofauti iliyo wazi ikichorwa kati ya jina la Baba, la Mwana, na lile la Roho Mtakatifu katika Mathayo 28:19, ambapo twasoma, 'Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.' Tofauti ya Roho Mtakatifu na Baba na Mwana yadhihirika tena kwa uwazi mkubwa katika Yohana 14:16, ambapo twasoma, 'Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.' Hapa twamwona Nafsi mmoja, Mwana, akimwomba Nafsi mwingine, Baba, na Baba ambaye kwake aomba akimtoa Nafsi mwingine, Mfariji mwingine, kwa kuijibu sala ya Nafsi wa pili, Mwana.

Kama maneno yana maana yo yote, na kwa hakika katika Biblia yana maana ya yale yanenayo, hakuna kukosea kwamba Baba, Mwana, na Roho ni Nafsi tatu tofauti na za peke yake. Tena, katika Yohana 16:7, tofauti iliyo wazi yachorwa kati ya Yesu, aendaye zake kwa Baba, na Roho Mtakatifu, ajaye kutoka kwa Baba kuchukua mahali pake. Yesu asema, 'Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa sababu mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.'

Tofauti kama hiyo yachorwa katika Matendo 2:33, ambapo twasoma, 'Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.' Katika fungu hili, tofauti iliyo wazi kabisa yachorwa kati ya Mwana aliyepandishwa hata mkono wa kuume wa Baba na Baba ambaye kwenye mkono wake wa kuume amepandishwa, na Roho Mtakatifu ambaye Mwana ampokea kutoka kwa Baba na kumwaga juu ya Kanisa.

Kwa kufupisha yote, Biblia yachora tofauti iliyo wazi kabisa kati ya Nafsi tatu: Roho Mtakatifu, Baba, na Mwana. Ni unafsi tatu tofauti, wenye mahusiano kati yao kwa kila mmoja, wakitenda mmoja juu ya mwingine, wakinena juu ya au kwa mmoja na mwingine, wakitumia viwakilishi vya nafsi ya pili na ya tatu kwa mmoja na mwingine.

Ukurasa 1 / 2 · 3 dakika zimebaki katika sura
Ochorus

Kuwawezesha watu vitabu vya Kikristo vya kale — bila malipo, kwa lugha yako.

Chunguza

Dhamira Yetu

Vitabu vya Kikristo vya kale bila malipo mtandaoni — na vitabu vilivyochapishwa tunavyogawa kwenye makongamano, makanisa, shule na magereza kote Afrika Mashariki.

Faragha na Masharti

Huduma tangu 2021 · Victoria BC, Kanada · Kampala, Uganda