Sura 16 · dakika 5 za kusoma
Yamefunuliwa kwa Watoto Wachanga
“Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.” Mathayo 11:25, Luka 10:21.
Wenye hekima na busara ni watu wenye kujua na kujiamini juu ya nguvu ya akili na fikira zao za kuwasaidia katika kufuatilia kwao Maarifa ya Kimungu. Watoto ni wale ambao kazi yao kuu si akili na nguvu yake, bali moyo na hulka yake. Ujinga, kutokuwa na msaada, kutegemea, upole, kufundishika, uaminifu na upendo—hizi ndizo hulka Mungu azitafutazo katika wale awafundishao. (Zaburi 25:9, 12, 14, 17, 20.)
Mmojawapo wa sehemu za muhimu zaidi za ibada zetu ni kujifunza neno la Mungu. La umuhimu wa kina ulioje kwamba tulipokee neno daima katika roho ingojayo Baba afunue kweli yake ndani yetu. Na la umuhimu ulioje kwamba tuwe na ile hulka ya kitoto, naam, ya kitoto ambayo Baba hupenda kuiaminisha siri za upendo wake. Kwa wenye hekima na busara maarifa ya kichwani ndilo jambo la kwanza; kutoka kwao, Mungu huficha maana ya kiroho ya kile kile wadhanicho wanakielewa.
Kwa watoto, si kichwa na maarifa yake bali moyo na hisia, ile hisi ya unyenyekevu, upendo na uaminifu, ndilo jambo la kwanza, na kwao Mungu hufunua, katika uzima na uzoefu wao wa ndani, kile kile wajuacho hawawezi kukielewa.
Elimu hutuambia kwamba kuna namna mbili za kufundisha. Mwalimu wa kawaida hufanya kutoa maarifa kuwa lengo lake kuu, na husitawisha nguvu za mtoto kadiri zinavyomsaidia kulifikia lengo lake. Mwalimu wa kweli huhesabu kiasi cha maarifa kuwa jambo la pili.
Lengo lake la kwanza ni kusitawisha nguvu ya akili na roho, na kumsaidia mwanafunzi, kiakili na kimaadili, kutumia nguvu zake vizuri, katika kufuatilia na kutumia maarifa. Vivyo hivyo kuna aina mbili za wahubiri. Wengine humimina mafundisho na hoja na sihi bila kukoma, wakiwaachia wasikiaji watumie vema wawezavyo yale yaletwayo kwao.
Mhubiri wa kweli hujua jinsi mengi yategemeavyo hali ya moyo, na hutafuta, kama vile Bwana wetu Yesu alivyofanya, kuweka mafundisho ya kweli au fundisho la nje chini ya kusitawisha zile hulka ambazo bila hizo mafundisho hufaidi kidogo. Mahubiri mia moja, yenye ufasaha na bidii, kwa wenye hekima na busara, kwa Wakristo wasikiao kwa wazo kwamba waweza kuelewa na kwamba wasikiacho kwa namna fulani kitawafaidi, yataleta baraka halisi ndogo, kuliko hubiri moja kwa wasikiaji ambao ndani yao mhubiri ameamsha ufahamu wa ujinga wa kiroho, roho ya kitoto ifundishikayo ingojayo na kutegemea, ipokeayo na kutii kwa kweli, mafundisho ya Baba.
Katika chumba cha siri kila mtu ni, kwa kadiri msaada wa kibinadamu unavyohusika, mwalimu na mhubiri wake mwenyewe. Yampasa kujifunza katika desturi ya baraka ya urahisi wa kitoto na kufundishika.
Akikumbuka kwamba haikuwa tu ya lazima kwamba Kweli ya Kimungu ifunuliwe ulimwenguni, bali kwamba lazima uwepo ufunuo binafsi kwa kila mmoja, kwa Roho Mtakatifu, hangaiko lake la kwanza ni kumngoja Baba amfunulie, na ndani yake, siri iliyofichwa katika nguvu yake katika uzima wa ndani. Katika hali hii, hutumia roho ya kitoto, na kuupokea Ufalme kama mtoto mdogo. Wakristo wote wa Kiinjili huamini kuzaliwa mara ya pili.
Ni wachache kiasi gani waaminio kwamba mtu azaliwapo na Mungu, utegemezi wa kitoto juu ya Mungu kwa mafundisho na nguvu yote wapaswa kuwa sifa yake kuu. Ilikuwa jambo moja Bwana wetu Yesu alilolisisitiza zaidi ya yote. Alipowatangaza maskini wa roho, wapole, wenye njaa, kuwa “heri,” aliwaitapo watu wajifunze kwake kwamba yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, aliponena mara nyingi juu ya kujinyenyekesha na kuwa kama watoto wadogo, ilikuwa kwa sababu alama ya kwanza na kuu ya kuwa mtoto wa Mungu, ya kuwa kama Yesu Kristo, ni kumtegemea Mungu kabisa kwa kila baraka, na hasa kwa maarifa yoyote halisi ya mambo ya kiroho. Kila mmoja na ajiulize: Je, nimeihesabu roho ya kitoto kuwa jambo la kwanza la lazima katika kujifunza kwangu Biblia? Kujifunza Biblia kwa faida gani bila roho ya kitoto? Ndio ufunguo halisi na pekee wa shule ya Mungu.
Je, isingekuwa vema kuweka kando kila kitu ili kuhakikisha hili? Ndipo tu Mungu atakapofunua hekima yake iliyofichwa.
Kuzaliwa upya, kuzaliwa na Mungu, ambako kwako twakuwa watoto wa Mungu, kumekusudiwa kutufanya watoto wachanga. Kutatupa roho ya mtoto pamoja na mafundisho ya mtoto. Hakuwezi kufanya la pili bila la kwanza. Na tuamini na kujitoa kwa uzima mpya ulio ndani yetu, kwa uongozi wa Roho; atapumua ndani yetu roho ya watoto wachanga. Lengo la kwanza la kujifunza Biblia ni kujifunza hekima ya Mungu iliyofichwa. Sharti la kwanza la kupata maarifa haya ni kukubali ukweli kwamba Mungu Mwenyewe hutufunulia. Sharti la kwanza la kupata maarifa haya, ni kukubali ukweli kwamba Mungu Mwenyewe hutufunulia.
Hulka ya kwanza inayohitajika kwa kupokea ufunuo huo ni roho ya kitoto. Sote twajua jinsi jambo la kwanza mfanyakazi mwenye hekima alifanyalo ni kuona kwamba ana vifaa vinavyofaa, na kwamba viko katika hali nzuri. Hahesabu kuwa muda umepotea kusimamisha kazi yake na kunoa vifaa. Si muda uliopotea kuacha kujifunza Biblia kungoje, hadi utakapoona kama uko katika hali ipasayo—ukingoja ufunuo wa Baba katika roho ya upole na ya kitoto.
Ukihisi kwamba hujaisoma Biblia yako katika roho hii, ungama na uache mara moja roho ya kujiamini ya wenye hekima na busara. Si tu omba roho ya kitoto, bali iamini. Imo ndani yako, ijapokuwa imepuuzwa na kukandamizwa; waweza kuanza mara moja kama mtoto wa Mungu kuionja.
Usitafute kwa tafakuri au hoja kuleta roho hii ya kitoto moyoni mwako. Fanya kazi toka ndani kwenda nje.
Imo ndani yako, kama mbegu, katika uzima mpya, uliozaliwa na Roho. Lazima iinuke na kukua ndani yako kama uzao wa Roho akaaye ndani. Katika imani hii, si tu upaswa kuomba, bali omba pia hasa kwa ajili ya neema hii ya Roho, na kuitumia. Ishi kama mtoto mchanga mbele za Mungu. Kama mtoto aliyezaliwa sasa autamaniavyo maziwa ya Neno. Na ujihadhari na kujaribu kuchukua hali hii ya nia tu unapotaka kujifunza Maandiko. Lazima iwe desturi ya kudumu ya nia yako, hali ya moyo wako. Ndipo tu utakapoweza kufurahia uongozi wa daima wa Roho Mtakatifu.