Sura 2 · dakika 1 za kusoma
Dibaji ya Keith Price
Hakika hakuwezi kuwa na pendekezo bora kwa kitabu kuliko kuwa kimestahimili mtihani wa jaribio la kimatibabu. Kwamba mtihani wa namna hiyo umetumika kwa kanuni zinazoelezwa hapa ni hakika uthibitisho wa kutosha.
Unaposoma kurasa hizi utahisi moyo wa mchungaji.
Ingawa ni mtu wa sayansi, mtu huyu wa Mungu hana wakati wa minara ya pembe za ndovu. Baada ya kupita mwenyewe katika moto wa mikwaruzo ya maisha yenye milima mirefu, anaelewa jinsi wengine wanavyohisi katika nyakati za taabu.
Gareth Evans amezithibitisha kanuni hizi si tu katika kazi ya kichungaji huko Victoria, British Columbia, bali pia mbali zaidi katika maeneo tofauti tofauti kama Mexico, Afrika, Ulaya, na Australia ambako amealikwa kuwasilisha mafundisho haya kwa vikundi vingi mbalimbali vya makanisa na viongozi wa Kikristo.
Kwa sababu ya uthamini wake mkubwa wa uvuvio wa maandiko ambamo anachota mafunzo haya, nina uhakika kwamba yatabaki na thamani yake hadi sisi, tukiwa tumekamilishwa, tusipohitaji tena kuchukua hatua ya kwanza kurejesha uhusiano uliovunjika.
Keith Price Victoria, British Columbia Machi, 1996