Kumfuasa Kristo
Kuepuka mazoea yaliyopita kiasi

Sura 9 · dakika 1 za kusoma · dakika 1 za kusikiliza

Kuepuka mazoea yaliyopita kiasi

USIMFUNULIE kila mtu moyo wako, bali jadili mambo yako na mtu mwenye hekima na anayemcha Mungu. Usiandamane na vijana na wageni. Usiwabembeleze matajiri, wala usipende kuchanganyika na wakuu. Shirikiana na wanyenyekevu na watu sahili, na wacha Mungu na wenye wema, na pamoja nao zungumza mambo ya kujenga. Usiwe na urafiki wa karibu na mwanamke yeyote, bali kwa jumla wakabidhi wanawake wote wema kwa Mungu. Tafuta urafiki wa karibu na Mungu tu na malaika zake, na uepuke kuonwa na wanadamu.

Tunapaswa kuwa na upendo kwa watu wote, lakini kuzoeana sana na wote hakufai. Wakati mwingine hutokea kwamba mtu anafurahia sifa njema miongoni mwa wale wasiomjua, lakini wakati huo huo anaheshimiwa kidogo na wale wanaomjua. Mara nyingi tunadhani kwamba tunawapendeza wengine kwa kuwapo kwetu, kumbe tunaanza zaidi kuwachukiza kwa sababu ya makosa wanayoyaona ndani yetu.

Umemaliza Kuepuka mazoea yaliyopita kiasi