Sura 2 · dakika 4 za kusoma

Umuhimu Wa Maombi

Mara utakapofahamu jinsi jambo fulani lilivyo la ajabu, hutaweza kulazimishwa ili ulitamani!

Kuna wingi wa faida za maombi. Kwako wewe mwanafunzi, kufahamu jambo hili ni muhimu kwa sababu utaongozwa kujua la kutarajia. Kwa kujifunza jinsi ya kuomba, roho yako itawashwa moto kuomba zaidi kuliko wakati wowote. Unaposoma yaliyomo katika sura hii, acha moyo wako na roho yako viwe vinyenyekevu na wazi vya kutosha kuilisha roho yako. Tazama umuhimu huu wa maombi, na acha roho yako ifurahi sana!

1. Maombi hutusaidia kuwa na ushirika na Mungu. Ni jambo zuri kama nini kuwa kitu kimoja na Mungu, kuunganishwa na Muumba wa vitu vyote, ukijua yaliyo moyoni mwake na ukijua hasa jinsi unavyoweza kutimiza matakwa yake hapa duniani. Hili ni la ajabu mno!

2. Je, ulijua kwamba wakati mwingine watu hawapati adhabu kutokana na matendo yao kwa sababu mtu fulani au watu fulani wamemwomba Mungu awahurumie hawa wenye hatia? Ndivyo maombi yalivyo na nguvu! Baba yako, Mama yako, ndugu au rafiki yeyote wanaweza kuwa wamefanya jambo ambalo hata hufikirii Mungu anaweza kulisamehe; jambo kubwa ambalo ulimwengu wote unaweza kuwa kinyume nalo, lakini kupitia maombi, unaweza kumwomba Mungu awahurumie, naye Mungu husikia tunapoomba. Mungu anaweza kuwaokoa jamaa na rafiki zako kutokana na adhabu ambayo wangeipata kwa ajili ya matendo yao. Utukufu kwa Mungu! Hapa kuna mfano mzuri sana katika Biblia ambapo Yesu alimwomba Mungu, na maisha yakasamehewa.

“Hata walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo wakamsulubisha huko, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” Luka 23:33-34.

Basi, kama unaye mtu ambaye ungependa Mungu amsamehe, endelea kumwombea. Mungu anaweza kumhurumia na hata kuiondoa adhabu ambayo angeipata kama usingeomba.

3. Umuhimu mwingine wa maombi ni kwamba hutusaidia kumkazia macho Mungu.

“Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.” Wakolosai 3:2. Tunaweza kuyafikiri yaliyo juu kupitia maombi kwa sababu maombi hutusaidia kukaza fikira, na kuona yale ambayo Mungu huyaona. Mwanadamu na Mungu ni roho, hivyo katika maombi, unakaza fikira juu ya mambo ya kiroho kwa sababu uko katika ushirika na Mungu, ambaye ni Roho.

4. Tunapoomba, Roho Mtakatifu naye hutupatia maagizo na uongozi. Warumi 8:26 husema, “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”

Kwa kuwa Roho Mtakatifu anayajua mapenzi ya Baba aliye Mbinguni, hutusaidia kuyaeleza mapenzi ya Baba, na hivyo, tunapokea uongozi wa jinsi ya kuyatimiza au kuyatenda mapenzi ya Mungu kwa mafanikio. Je, hilo si zuri? Bila Roho Mtakatifu, haiwezekani kuyaelewa kikamilifu mapenzi ya Mungu.

Matendo 13:2 hutuonyesha jinsi wanafunzi walivyopokea maagizo kutoka kwa Roho Mtakatifu walipokuwa katika ushirika naye.

“Basi walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akanena, “Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.”

Ndiyo maana kila Mkristo anapaswa kumzingatia Roho Mtakatifu na kumsikiliza.

Unapoomba, mruhusu Roho Mtakatifu akuongoze kwa sababu anayajua yale ambayo Mungu anataka na yale unayohitaji.

5. Katika maombi, tunashinda! Haleluya! Ahimidiwe Mungu! Kama Mkristo, ni muhimu kujua kwamba kila kinachotokea katika ulimwengu wa mwili hutokea kwanza katika ulimwengu wa roho. Tunapoomba, Mungu hutuimarisha. Tuna nguvu maalum kutoka kwake inayotusaidia kufanikiwa na kuwa na afya njema. Nguvu hii hutuwezesha kukanyaga vitu vya hatari, kutoa pepo kwa jina la Yesu, na kufanya mambo yanayoonekana kuwa hayawezekani kwa wengine.

Je, unakabiliwa na tatizo? Omba na uamini kwamba mambo yataendelea kuwa mazuri kila siku. Mungu husikiliza tunapoomba, naye hujibu. Ana mipango mizuri kwa ajili yetu, naye hutusaidia kuyashinda hata magumu makubwa kupita yote.

6. Maombi hututia nanga. Kama Wakristo, hatuombi ili kumfanya Mungu abadilike— yeye habadiliki kamwe.

Pia hatuombi ili kupata usikivu wake kwa sababu tayari sisi ni wa maana kwake. Sikuzote tuko machoni pake. Msifuni Mungu! Badala yake, maombi hutusaidia kumkazia macho yeye. Hutukumbusha kwamba tuko salama pamoja naye, hali yoyote ile. Ndiyo maana ni muhimu sana kuomba wakati wote, ili tusikate tamaa wala kupoteza tumaini, bali tuendelee kuwa tumeunganishwa na Mungu. Tazama andiko hili katika Luka 18:1, “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kuomba sikuzote, wala wasikate tamaa.”

7. Tunapoomba, tunaweza kuyanena mambo yakawepo. Maisha yako ni jukumu lako, naye Mungu amekupa Roho Mtakatifu na Neno lake ili uweze kuumba ulimwengu wako. Wewe ni nani na yale unayoyapitia ni matokeo ya maneno yako. Kwa Neno la Mungu, unaweza kubadilisha hali na kuumba vitu vipya.

Mungu alipokuumba, alikuumba kwa mfano wake mwenyewe, jambo ambalo lina maana kwamba anataka uwe kama yeye — muumbaji. Una uwezo wa kuumba hali yako mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kukataa kuugua kwa sababu yule ambaye unabeba mfano wake (Mungu) hawezi kamwe kuugua. Unaweza kuchagua kuishi maisha mazuri kila siku, bila kujali unavyojihisi.

Watu wengine husema maisha yana kupanda na kushuka, lakini mimi huwauliza, "Biblia inasema wapi hivyo?" Sivyo inavyopaswa kuwa kwa mwamini. Mara nilipoijua kweli, maisha yangu yamekuwa yakipanda na kusonga mbele tu! Msifuni Bwana! Una mamlaka juu ya maisha yako na kila kilichomo ndani yake. Inawezekana kuishi maisha ya mafanikio yasiyokoma, majira baada ya majira, mwaka baada ya mwaka.

Yanene maisha yako na uyatumie yale ambayo Mungu amekupa. Kumbuka, Mungu hataki uandike Biblia mpya; anataka ulielewe Neno lake na uishi kwa kulifuata. Tangaza ufanisi na wingi kwa kinywa chako mwenyewe kwa sababu wewe ndiye nabii wa maisha yako mwenyewe! Haleluya!

Ukurasa 1 / 4 · 4 dakika zimebaki katika sura
Ochorus

Kuwawezesha watu vitabu vya Kikristo vya kale — bila malipo, kwa lugha yako.

Chunguza

Dhamira Yetu

Vitabu vya Kikristo vya kale bila malipo mtandaoni — na vitabu vilivyochapishwa tunavyogawa kwenye makongamano, makanisa, shule na magereza kote Afrika Mashariki.

Faragha na Masharti

Huduma tangu 2021 · Victoria BC, Kanada · Kampala, Uganda