Waraka wa Kwanza wa Clement kwa Wakorintho
Tuuhifadhi Kanisani utaratibu aliouweka Mungu

Sura 40 · dakika 1 za kusoma · dakika 1 za kusikiliza

Tuuhifadhi Kanisani utaratibu aliouweka Mungu

Basi kwa kuwa mambo haya yamekuwa wazi kwetu, na kwa kuwa tunachungulia vilindi vya maarifa ya Mungu, imetupasa kufanya mambo yote kwa utaratibu [wake unaofaa], ambao Bwana ametuamuru kuutimiza kwa nyakati zilizowekwa. Ameagiza matoleo [yatolewe] na ibada ifanyike [kwake], tena si kwa uzembe wala bila utaratibu, bali kwa nyakati na saa zilizoamriwa. Mahali yatakapofanyika mambo haya, na ni nani atakayeyafanya, Yeye mwenyewe ameyaweka kwa mapenzi yake makuu, ili mambo yote yakitendwa kwa utauwa kama apendavyo, yapate kukubalika kwake. Basi wale watoao matoleo yao kwa nyakati zilizowekwa hukubaliwa na kubarikiwa; kwa maana, kwa kuwa wanazifuata sheria za Bwana, hawatendi dhambi. Kwa maana kuhani mkuu amepewa huduma zake mwenyewe za pekee, na makuhani wameandikiwa mahali pao wenyewe, na Walawi wamekabidhiwa huduma zao maalum. Mtu wa kawaida asiye kuhani amefungwa na sheria zinazowahusu watu wa kawaida.

Umemaliza Tuuhifadhi Kanisani utaratibu aliouweka Mungu