Sura 27 · dakika 1 za kusoma · dakika 1 za kusikiliza
Katika tumaini la ufufuo
Basi tukiwa na tumaini hili, nafsi zetu na zifungamane naye aliye mwaminifu katika ahadi zake, na mwenye haki katika hukumu zake. Yeye aliyetuamuru tusiseme uongo, zaidi sana yeye mwenyewe hatasema uongo; kwa maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu, isipokuwa kusema uongo. Basi imani yake na iamshwe tena ndani yetu, na tufikiri kwamba vitu vyote vi karibu naye. Kwa neno la uweza wake alivisimamisha vitu vyote, na kwa neno lake aweza kuviangusha. “Ni nani atakayemwambia, Umefanya nini? au, Ni nani atakayeshindana na uweza wa nguvu zake?” Wakati apendapo na kama apendavyo atayatenda mambo yote, wala hakuna lolote kati ya yale aliyoyaamua litakalopita. Vitu vyote vi wazi mbele zake, wala hakuna kitu kiwezacho kufichika kwa shauri lake. “Mbingu zahubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, na usiku huhubiriana maarifa na usiku. Wala hakuna maneno wala lugha ambayo sauti zao hazisikiki.”