Sura 22 · dakika 1 za kusoma · dakika 1 za kusikiliza
Mawaidha haya yanathibitishwa na imani ya Kikristo
Basi imani iliyo katika Kristo inayathibitisha [mawaidha] haya yote. Kwa maana yeye mwenyewe kwa Roho Mtakatifu anatuambia hivi: “Njoni, enyi wana, mnisikilize; nitawafundisha kumcha Bwana. Ni nani mtu yule apendaye uzima, apendaye kuona siku njema? Uuzuie ulimi wako na mabaya, na midomo yako na kusema hila. Uache mabaya, ukatende mema; utafute amani, ukaifuatie. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake [yako wazi] kwa maombi yao. Uso wa Bwana ni juu ya watendao mabaya, ili kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. Mwenye haki alilia, naye Bwana akamsikia, akamwokoa na taabu zake zote.” “Mapigo [aliyowekewa] mtu mwovu ni mengi; bali rehema zitawazunguka wale wamtumainio Bwana.”